MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Ndoa

Hapana hata sikuwa nimeolewa, this was the very first day i meant my Husband @ the Church

Wakati mgumu katika maisha ya kijana wa kike au wa kiume ni pale anapotaka kumpata mwenzi wake wa maisha. Vijana wengi wanachanganyikiwa. Moja ya maeno yaliyokumbwa na uvunjifu mkubwa wa maadili ni uchumba hadi ndoa na limeathiri moja kwa moja Ndoa na Nyumba.

Kupata mme au Mke Sahihi- Mambo yanayosababisha utata katika kujua yupi ni jibu la Mungu:- Mwanzo 24:10-32
1.       Kutokuwa mtu sahihi: Wengi wanatafuta mtu sahihi- mzuri wa Mungu bila kwanza kuangalia wao kama ni watu sahihi. Kama wewe kijana- Hukujitoa kwa Mungu, wokovu wako ni wa wasiwasi, Roho Mtakatifu huna, maisha yako ni ya mchanganyiko, kuomba huwezi, ibada mvivu, Unajisumbua kupata mke au mme sahihi kutoka kwa Mungu.
“If a Child of God marries a child of the devil, the said child of God is sure to have trouble with his father in Law”

2.       Kutafuta mtu asiye sahihi: Vijana wengi wamejikuta wanatafuta mtu asiye sahihi bila wao kujielewa kuwa wanatafuta asiye sahihi- wao wanadhani watafuta mtu aliye sahihi. Wanaanza kwa kuwa na picha ya mtu Fulani katika aliki na ufahamu wao wa mtu wanayedhani kuwa ni sahihi- Wanamtengeneza kwa kuorodhesha sifa nyingi za kimwili wanazozitaka hadi zinaumba mtu hewa ndani ya fahamu zao ndipo wanaanza kumwomba Mungu awape huyo waliyemtengeneza kichwani.

“To marry a Woman for her Look is eating a bird for it song. Since you do not marry her look but to have as a companion and helpmeet. Observe the formation of her mind as well as the features of her face“.

Pamoja na mambo muhimu wanayotakiwa kujua kuhusu huyo atakaye kuwa mwenzi wako lakiniusiumbe mtu akilini mwako.

3.       Kuwa na nia isiyo sahihi au mtazamo usio sahihi: Baadhi ya sababu zisizo sahihi kwa nini unaoa ni:-
a.)    Baadhi ya vijana wanajiona wamechelewa baada ya kuona wenzao wote wameoa au kuolewa- (Peer Pressure) anahamaki anaona afadhali nay eye aoe au aolewe- Hiyo si babu sahihi
b.)    Kukimbia mazingira mabaya au magumu ya nyumbani- Mwingine anaamua afadhali aolewe. Baada ya kuona hali ya maisha ni ngumu
c.)     Wengine wanalazimisha kuolewa baada ya kuona tatizo na uchumba wa kawanza kuvunjika – anataka kuziba pengo au kulipa kisasi.
d.)     Msukumo wa wazazi wa kimwili au hata kiroho – unaweza kumfanya kijana akachanganyikiwa akaamua kumkubali mtu bila uhakika wa mapenzi ya Mungu. Usikubali Msukumo wowote hata kama ni wa mtu mkubwa kiasi gani – Utakuja juta Milele – Tafuta Mapenzi ya Mungu.
e.)    Wengine wanaamua kuolewa ili kupata mahitaji yake- Mshahara hautoshi, ngoja nioe ili fesha iongezeke. Mahitaji haya yanaweza kuwa- Heshima, Mapenzi, Kishisia nk
f.)     Wengine wanalazimika kuoa au kuolewa baada ya kufanya ujinga na mimba kutokea- Lazima umuoe au uloewe naye.


Itaendelea
by: Nicelynee Kennedy
Kwa maswali au Ushauri:
Tuma Email: nicekennedy@gmail.com
Andika Barua kwa Nice Kennedy Hillary
C/o Assemblies of God Press Printings
P.O.BOX 60411, Dar es Salaam
Tanzania
Simu: +255 768 444 555

Comments

Popular posts from this blog

Benny Hinn Wedding Ceremony Pictures

Mkutano wa Injili na Semina ya Pasaka